Kama mdau wa blogu hii napenda wasomaji wa blogu hii kusoma taarifa hii kuhusu lishe bora hasa kwa wagonjwa wa magonjwa sugu yasiyoambukiza kama kisukari, pressure, saratani, ugonjwa wa figo nk.
Magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kufuata mtindo bora wa maisha. Mtindo bora wa maisha ni muhimu katika kuendeleza na kudumisha afya ya mtu na kuzuia maradhi, hususani magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji unaofaa, kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, kuepuka matumizi ya pombe, na kuepuka msongo wa mawazo
Kwa habari zaidi soma nyaraka hii.